MHESHIMIWA DK DAMAS DANIEL NDUMBARO, WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA
MHESHIMIWA JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA YA RUFANI JUSTICE JANUARY MSOFFE, MWENYEKITI WA TUME YA KUBADILISHA SHERIA
MHESHIMIWA FELISTA LELO, SENIOR STATE ATTORNEY ALIYE MWAKILISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI,
WAADHIRI WA VYUO MBALI MBALI NCHINI,
MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA,
WAHESHIMIWA MAWAKILI WOTE WA SERKALI,
WAHESHIMIWA MAWAKILI WOTE WA KUJITEGEMEA,
WAKUU WA TAASISI MBALIMBALI NCHINI,
WAGENI WOTE WAALIKWA
MABIBI NA MABWANA
NDUGU MGENI RASMI,
Awali ya yote, napenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kufika hapa nikiwa na afya njema kwa ajili ya maharaniwa kitabu hiki kinachofahamika kama “Comprehensive Employment and Labour Laws: Practise in Modern Business” nilichokiandika kwa Zaidi ya miaka mitano. Ni siku ya furaha kwa kuweza kutimiza ndoto yangu ya muda mrefu.
Lakini kabla sijaendelea ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa Mgeni Rasmi, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dk. Damas Ndumbaro kwa kukubali kunizndulia kitabu hiki na kukubali kujumuika nasi. Nashukuru sana.
Kwa dhati kabisa nawashukuru viongozi wote waliofika na watendaji wa sehemu mbalimbali katika tassisi na mawakili wenzangu kwa kufika kwenu katika siku hii ya uzinduzi wa kitabu change.
Shukrani kubwa imuendee Prof Chris Maina Peter kwa ushauri wake katika safari yangu ya elimu na hasa katika kunihimiza kubadili fani na kusoma sheria. Shukurani hizi ni za kipekee kwa kuwa muongozo wake, hasa yake na ushauri wake ndiye ulinifanya kufikia hatua hii na hadi sasa ni mkufunzi katika Shahada ya Uzamivu, katika Chuo cha Huria, Dar es Salaam. Lakini bila kusahau Prof Peter ndiye mmoja katika ya watu waliyonihamasisha kuandika katika tasnia ya sheria na bila yeye siku ya leo isingeweza kutimia.
Kwa kiwango kikubwa pia ningependa kuwashukuru wafanyakazi wenzangu wa MDM Law Group kwa kufanya nami kazi kubwa sana ya kunisaidia katika tafiti mbalimbali za kuandika kitabu hiki. Ninawashukuru sana.
Lakini mwisho ninaishukuru sana familia yangu mke wangu Pamoja na Watoto wangu kwa kunivumilia katika kipindi chote cha uandishi wa kitabu hiki.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila nikishindwa kuishukuru kampuni ya Lexis Nexis ya Afrika Kusini kwa kazi kubwa ya uhariri na mpangilio wa kazi hii.
Asanteni sana.
NDUGU MGENI RASMI
Safari yangu ya elimu imekuwa ndefu sana na ninakumbuka wakati wa ujana wangu sikuwahi kupata hamasa ya kuwa mwanasheria lakini baada ya kushauriwa basi nilipata kujiunga na Chuo Kikuu cha Tumaini ambapo nilisoma shahada yangu ya sheria. Na ni katika kusoma sheria ndipo kwa mapito yangu ya nyuma ya ajira yakanifanya kutambua mapungufu makubwa katika Sheria za Mahusiano Kazini kati ya mwajiri mwajiriwa. Uelewa huu ndio ulionipa hamasa ya kuandika kitabu hiki.
NDUGU MGENI RASMI
Kupitia kitabu hiki nimeweza kuelezea kwa mtazamo wa sheria na pia kwa mtazamo wangu masuala mbali mbali ya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini kuanzia historia ya ajira nchini, mabadiliko ya sheria za ajira na mahusiano kazini mwaka 2006, na taratibu zote za ajira kuanzia kuingia mkataba wa ajira, aina za mikataba ya ajira, kanuni za ajira, maswala ya nidhamu katika sehemu ya kazi, hatua za kuchukuliwa iwapo mfanyakazi atakiuka kanuni za kazi na mambo mengine mengi yahusuyo ajira. Nikieleza yote hapa siwezi kumaliza na ukubwa wa kitabu unaweza kuwa shahidi katika hili.
NDUGU MGENI RASMI
Lakini kikubwa na cha tofauti katika kitabu hiki ni uchambuzi wa kina uliyofanyika katika ya Sheria ya Mahusiano Kazini na Sheria ya Utumishi wa Umma baada ya mabadiliko makubwa yaliyofanyika mwaka 2018 kwa kuwaondoka watumishi wote wa shirika, taasisi nk inayomilikiwa na serikali kutumia institutional framework za sheria ya kazi nchini bali kuwalazimu kutumia Tume ya Utumishi wa Umma kama ndiyo mwenye mamlaka ya kutatua migogoro ya kikazi ya watumishi hawa. Hii ni hatua kubwa ya mabadiliko iliyoletwa na serikali na uchambuzi wa kina umefanyika katika kuleta na kuonyesha tofauti hizi.
NDUGU MGENI RASMI
Tanzania ya sasa inakua kichumi kwa kasi baada ya juhudi mbalimbali zinazoendelea kufanyika na serikali. Wawekezaji mbalimbali wanaingina nchini wanaweza kutumia kitabu hiki kama muongozo wa kina wa namna ya kuajiri wageni na wenyeji katika kampuni zao. Taratibu za kuhusu namna ya kuomba vibali vya kazi na makazi ime elezewa kwa kina n ani matumaini yangu kwaba makampuni haya kwa kutumia kitabu hiki watapata majibu ya maswali yao.
NDUGU MGENI RASMI,
Lakini pia wanatasnia wenzangu kazi za uandishi wa vitabu vya sheria imeachiwa wanataaluma. Practitioners kwa sasa ni wachache wenye ari na hamasa ya kuandika vitabu. Niwahamasishe mawakili wenzangu kutumia elimu zetu katika kuelemisha jamii na katika kuirahisishia tafsiri ya sheria zetu. Hii inakuwa pia ni namna yak u-diversify profession na kuwa chanzo kingine cha mapato kwetu sisi.
NDUGU MGENI RASMI,
Nita kuwa sijamaliza kuzungumza bila kuwa zungumzia young and aspiring lawyers out there. Hii taaluma ni yetu sote. Tuungane mkono tushirikiane ilikuweza kuwahudumia watanzania wenzetu wenye uhitaji wa taaluma yetu kwa kuwapa huduma bora iliyojaa uweledi ilituweze kufanikisha malengo yetu. True development is self development. Tukifanya hivi tutakuwa tunaweza kusimama kifua mbele na kuheshimika katika jamii.
NDUGU MGENI RASMI,
Kwa kumalizia ninapenda kusistiza ajira ni jambo nyeti sana kwa maendeleo ya taifa, jamii na mtu moja moja. Ajira imekuwa chanzo cha ujira duniani kote. Kama umeajiriwa kwenye sekta ya umma au binafsi au unafanya shuguli zako binafsi basi nayo ni ajira. Ili kila mwananchi anufaike na uchumi wa nchi ukue ni lazima kuwe na uzalishaji na ufanyaji kazi kwa bidii ambayo kimsingi ndio ajira. Bila nguvu kazi watu hakuna maendeleo ya kiuchumi yatapatikana katika nchi, hivyo basi rasilimali watu ni muhimu sana kwa taifa la leo na ndio mada kuu ya kitabu changu.
NDUGU MGENI RASMI,
Ni matumaini yangu kwamba matumizi ya kitabu hiki yataleta matokeo chanya katika practice na atakaye kitumia atanufaika sana na uchambuzi mbalimbali uliyofanyika. Lakini pia watunga sera, wabunge na serikali kwa ujumla pia watajifunza jambo kwa kuwa ushauri mbalimbali katika maeneo tofauti ya ajira zimejadiliwa kwa kina na iwapo watapata fursa ya kusoma ya kukisoma kitabu hiki basi wataweza kupata majibu ya maswali ambayo yalikuwa yanawatatiza kwa muda mrefu.
Niwahamasishe kila mmoja wenu aondoke leo na nakala yake.
NDUGU MGENI RASMI
Nimalizie kwa nukuu ya Eleanor Roosevelt aliyesema “The future belongs to those who believe in the beauty of their dreams.” Niliota ndoto ya kuandika kitabu na ndoto hii leo imetimia. Nina amini kwamba ndoto zangu zitaendelea kutimia kwa kuwa nina amini katika ndoto zangu. Ndoto ambazo familia yangu, ndugu, jamaa, marafiki, wanataaluma, wanasheria wenzangu wamenifanya nizitimize. Ninawashukuru sana.
Namshukuru Mungu na nina washukuru kwa kunisikiliza.
Asanteni sana